MKurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi,Bwa.Ruge Mutahaba kwa niaba ya uongozi wa
Clouds Media Group na PrimeTime Promotions Ltd ambao ndio waandaaji wa
Tamasha la Fiesta 2014,ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo
lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika kesho
jumapili ndani ya uwanja wa Karume.
Tamasha
hilo la Fiesta lilipangwa kufanyika JANA ijumaa mjini Musoma mkoani
Mara lakini kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo jana na
kusababisho vifo vya watu zaidi ya 40,iliyotokea katika kijiji cha
Sabasaba,wilaya ya Butiama mkoani Mara lilisitishwa ili kwenda sambamba
na tukio zima katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji
vyake,kutoa mkono wa pole,ambapo Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha
hilo na Waandaaji walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali
kusaidia majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.