Rapper
Azma Mponda ameamua kujitolea kupitia ngoma yake kuwafunda wanaume
wenzake namna ya kuwafikisha wapenzi wao katika kilele cha raha wakati
wa tendo maarufu zaidi duniani, ngono.
Akiongea
na Mpekuzi, Azma amesema ameamua kuachia wimbo wake huo uitwao ‘Jinsi
ya Kumkifikisha Mpenzi Wako Kileleni’, baada ya kuona amekuwa akifanya
nyimbo zenye ujumbe wa kijamii kwa muda mrefu lakini watu wanazichukulia
poa.
“Kikubwa
nimeona nimefanya kazi nyingi sana zenye ujumbe mkubwa mfano ‘Mungu
Inusuru Tanzania’, ‘Utata wa Katiba’, ‘Wanasubiri Nife’, ‘Kuwa na Azma’,
‘Kila Kitu Kila Siku’, ambayo nimerelease last week lakini ndo mapokeo
yake ni madogo.
“Ndio
maana nimeona nifanye kitu kingine ambacho kiko negative ili nipime
fikira za Watanzania pengine wanaweza kuvalue kazi kubwa ninayofanya,” amesema Azma.
Tazama video hapo chini