Advertisement

Responsive Advertisement

AJALI YAUA WANNE BAADA YA LORI KUGONGANA NA BASI HUKO IRINGA

Muonekano wa lori lenye namba za usajili T122 ALW baada ya kugongana na basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD katika kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD baada ya ajali hiyo.

Watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 20 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Panuel Express kugongana uso kwa uso na lori.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, akizungumza na NIPASHE jana alisema ajali hiyo ilitokea jana eneo la Idetero wilayani Mafinga saa 4:45 asubuhi.

Alisema basi hilo lenye namba za usajili T 969 BCD, lililokuwa likitoka mkoani Mbeya kwenda mkoani Dodoma.

Kamanda Mungi alilitaja lori lililogongana na basi hilo kuwa ni aina ya Scania T122 ALW likiwa na tela lenye namba za usajili T203 AKS mali ya Transco Company.

Alisema wakati basi hilo likielekea Iringa, mbele kulikuwa na lori bovu lenye namba za usajili T647 BAK lenye tela 388 AYF, mali ya kampuni ya Blue Fallcom ya jijini Dar es Salaam.

Alisema basi hilo liligongana na lori hilo wakati likitaka kulipita lori lingine lililokuwa limesimama barabarani na ndipo lilitokea lori lingine likitokea Mbeya na kukutana uso kwa uso.

Hata hivyo, alisema waliofariki dunia katika ajali hiyo majina yao bado hayajambuliwa huku majeruhi wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga kwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments