Wananchi
wa kijiji cha Nduoni kata ya kirua vunjo magharibi mkoani Kilimanjaro
wamefunga ofisi ya kijiji na kumpiga afisa mtendaji wa kata hiyo kwa
madai ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita kwa kumtangaza
mgombea wa chama cha mapinduzi kuwa mshindi badala ya mgombea wa chama
cha NCCR mageuzi.
Wananchi
hao walikusanyaika katika ofisi ya kijiji hicho wakiwa na mabango
mbalimbali na kusema kuwa wanasikitishwa na hatua ya serikali
kumwapisha mgombea wa chama cha mapinduzi Bw.Joseph Msaki aliyepata
kura 158 na kumwacha mgombea wa chama cha NCCR mageuzi Bw.Thomas Ngowi
aliyechaguliwa na wananchi kwa kupata kura 163.
Wamesema
wamefikia hatua ya kufunga ofisi hiyo kwa madai ya kupewa kiongozi
ambaye siyo chaguo la wananchi kwa kuwa serikali ilimwapisha kwa nguvu
mgombea wa chamacha mapinduzi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho
Kufuatia
vurugu za wananchi hao afisa mtendaji wa kata ya kirua vunjo magharibi
bw.reginald mlay alilazimika kumtangaza rasmi Bw.Thomas kupitia tiketi
ya chama cha NCCR mageuzi kuwa ndiye mshindi halali wa kijiji hicho
baada ya kupata kura 163 akifuatiwa na mgombea cha chamacha mapinduzi
aliyepata kura 158 na tlp kura tisa
0 Comments