Viongozi
wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza
ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es Salaam ya
kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini ambaye
alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili lakini
hadi leo amekaa kimya.
Mwenyekiti
wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema suala la
viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa anaposhindwa
kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia serikali hasara au
kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji ukawa ni kwa kila
mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa taifa.
Kwa
upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM
Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais atafanya
maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba suala
hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya baadhi
ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia
suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk
Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na kuenguliwa uteuzi wao
maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi kufikia hatua ya
kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio watuhumiwa wote
hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.
Katika
mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa Diamond
Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa
waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna Tibaijuka na
kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof Muhongo
0 Comments