Msanii
wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya
ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote
juu ya kitumbo hicho.
Akizungumza na mwandishi wetu, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.
Akizungumza na mwandishi wetu, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.
Alidai
kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu
wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi
kumuacha.
“Kiukweli
mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi
kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo
yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.
0 Comments