Mrembo
na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu amefunguka na kudai kuwa mwigizaji
Van Vicker wa Ghana, alichania kwa kiasi flani, kupelekea aachane na
aliekuwa mpenzi wake, Diamond.
Kwamujibu
wa GPL,akizungumzia sababu za kumwagana na Diamond, alisema pamoja na
sababu nyingine, Van Vicker alihusika kuwafanya wamwagane na mpenzi wake
huyo waliyedumu kwenye penzi zito lililokuwa gumzo kila kona ya Bongo.
“Kuna
vitu vingi vimechangia lakini Van pia amechangia, alianza ku-like picha
zangu, nikamwambia Dai (Diamond), akaniambia achana naye, baadaye
tulibadilishana namba, tukawa tunawasiliana.
“Ilipofika
wakati amenitaka tufanye kazi pamoja, nilipomwambia Diamond ndiyo
matatizo yalipoanzia hadi kufikia hatua ya kuachana,” aliweka nukta Wema.
0 Comments