MKAZI
wa Kitangiri jijini hapa, Biera Edwin (22) amelazwa katika Hospitali ya
Mkoa ya Sekou Toure akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya
sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mume wa mtu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola hakupatikana kuzungumzia
tukio hilo, lakini Biera mwenyewe alisema kabla ya kufanyiwa kitendo
hicho mama ambaye ni jirani yao alimtuma mtoto wake amwite nyumbani
kwao, alipokwenda mama huyo alianza kumshambulia.
Alisema
alimshambulia akishirikiana na marafiki zake na kumjeruhi vibaya kwa
nyaya za umeme, kumwingizia chupa kwenye sehemu zake za siri na baadaye
kuchoma nguo zake.
Binti
huyu kwa sasa amelazwa katika wadi ya majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa
wa Mwanza Sekou Toure akipatiwa matibabu na alisema baada ya kufanyiwa
ukatili huo pia waliteketeza nguo zake kwa moto.
Naye
dada wa majeruhi, Nice Cosmas anaeleza kuwa akiwa nyumbani kwao, mama
huyo wa jirani alituma watoto wake ambao walieleza kuwa wakamchukue mtu
wao.
Alisema walipokwenda hapo jirani alimkuta ndugu yake akiwa hana nguo huku akiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema
walilazimika kurudi nyumbani kumchukulia nguo za kumvisha na kisha
kutoa taarifa kwa mamlaka husika kabla ya kumpeleka hospitali kwa
matibabu.
Baadhi
ya viongozi wa mtaa wa Kitangiri A walisikitishwa na kitendo hicho na
kuomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali wahusika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri A, Issa Salum alisema wanataka haki itendeke kwani kitendo hicho ni nusu ya mauaji.
Naye
Mjumbe wa Serikali za Mitaa, Mariam Yusuf alisema mama huyo wa jirani
alipaswa kutoa taarifa kwa mabalozi ama kwa wazazi wa binti huyo kama
alikuwa na uhakika na madai yake kabla ya kuchukua ukatili dhidi ya
binti huyo.
0 Comments