Tembo walivamia kijiji kimoja India
wakiwa wanatafuta chakula, wakakuta kuna pombe ikiwa imewekwa na
wanakijiji kwenye makopo, wakanywa na kulewa.
Mbaya zaidi baada ya kulewa walianza
kufanya fujo, wakawa wanaangusha nguzo za umeme katika kijiji hicho na
baadaye tembo sita kati ya 40 walikufa baada ya kupigwa shoti na nyaya
za umeme.
Hii sio mara ya kwanza kwa tembo kufanya
tukio la namna hiyo, mwaka 2007 waliwahi kufa tembo wengine waliovamia
vijiji, wakanywa pombe na kufanya vurugu ikiwemo kuvunja nyumba za watu
na kukata nguzo za umeme.
0 Comments