Kaimu Kamnda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Juma Ndaki akionyesha baadhi ya wanahabari wa mkoani Tanga
(waliomzunguka) milipuko 475 ya Baruti iliyonaswa na askari wa doria
kwenye barabara kuu ya Mombo -Segera jana katika kijiji cha Chekelei cha
wilayani Korogwe ikiwa kwenye maboksi matatu ndani ya buti la basi
namba T. 491 ARB la kampuni ya Kilimanjaro Express lililokuwa likitoka
Arusha kuelekea jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Ndaki Milipuko hiyo
imekamtwa kwasababu ilikuwa inasafirisha isivyo halali (kinyume na
utaratibu) pasipo kuambatana na nyaraka zinazostahili kuambatana na
milipuko hiyo.
Aidha alisema kwa kuwa mhusika (mwenye
mzigo) hakuwepo eneo la tukio ilibidi askari kutumia mawasiliano ya
Kiintelijensia kupata taarifa zake ambapo muda mfupi baadae walibaini
kwamba mmiliki wa milipuko hiyo ni Efatar Edward Molel anaeishi eneo la
Kitianjala jijini Arusha.
Ndaki alisema tayari amekamatwa na
askari wa Arusha na anatarajiwa kukabidhiwa kwa jeshi la polisi la Mkoa
wa Tanga kesho kwakuwa taratibu za kumsafirisha zinaendelea.
Pichani
kushoto ni viroba 18 vya Mirungi vyenye uzito sawa na kilo 440 ambazo
zilikamatwa juzi na askari wa doria hapo Chekelei zikisafirishwa kwa
basi namba T 244 BXQ la kampuni ya Dar Express kutoka Arusha kwenda Dar.Kwa mujibu wa kaimu RPC wa Tanga, Juma Ndaki , Wakazi watatu wa jijini Dar es salaam wanashikiliwa kuhusu mirungi hiyo wakidaiwa kwamba ni wasafirishaji na wauzaji wa jumla wa bidhaa hiyo. Yumo Sara Mwambo(38), Robinson Sam (24) ambaye ni kondakta wa basi pamoja na Godfrey Machumbe (30) ambaye ni utingo wa basi hilo.
0 Comments