Wakazi wa kata ya Terrat wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia na kuzithamini huduma za
Afya na uzazi salama kwa kuwa ndiye mkombozi pekee kwa vifo vya mama
mjamzito mama mzazi mtoto Mchanga na mtoto chini ya miaka mitano katika
jamii.
Wito huo umetolewa na muuguzi
Msimamizi wa afya kitengo cha afya ya mama na mtoto zahanati ya Terrat
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara bibi Miriam Steven, wakati
akielezea namna ambavyo jamii hawazingatii na kuthamini umuhimu wa
huduma za afya kwa mama mzazi na mtoto ikiwa ni pamoja na
kutojifungulia katika vituo vya Afya.
Bi Miriam amesema kuwa wakazi wa kata
ya Terrat na maeneo jirani ambapo asilimia kubwa ni wafungaji wa jamii
ya kimasai wamekuwa wahudhuriaji wazuri wa Clinic wakati wa ujauzito na
kuwapeleka watoto Clinic lakini wakati wa kujifungua ujifungulia
nyumbani jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa mama na mtoto.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
hivi karibuni kwa njia ya simu, bibi Miriam amesema kuwa tatizo la
kuto kujifungulia zahanati kwa wamama wajawazito katika kata hiyo ni
kubwa, ikilinganishwa na mahudhurio ya Clinic wakati wa ujauzito
sambamba na upelekwaji wa watoto kupata huduma za Clini baada ya
kuzaliwa.
“ Tumekuwa tukipokea wajawazito na
watoto wengi sana kwa huduma za clinic tofauti na jinsi ambavyo akina
mama wanakuja kujifungulia katika zahanati yetu,tunachogundua wengi wa
kina mama hawa ujifungulia nyumbani na wengine wachache toka familia
zenye uwezo upelekwa mjini Arusha zaidi katika hosipitali ya akina mama
maarufu kama kwa Docta Wanjara iliyopo jiji humo, ni zaidi ya kilomita
85 kutoka hapa kijijini ” Alisema bibi Miriam.
Amesema kuwa kati ya wakina mama
wajawazito kumi wanaohudhuria huduma ya Clinik katika zahanati hiyo
wakati wa ujauziuzito mmoja kati yao ndiye anayejifukulia kituoni hapo
jamboo ambalo hata hivyo ni Nadra kutokea.
Bibi Miriam ameeleza sababu
zinazowafanya wakina mama wengi wa jami ya kifugsji kujifungulia
majumbani ni pamoja na mila na desturi za kuwaamini wakunga wa jadi,
sambamba na waume kutotilia maanani suala la huduma za afya ya uzazi
kwa kina mama la kuwasukuma kujifungulia katika vituo vya afya.
Aidha amesema kuwa wachache wanafika
kujifungua katika zahanati hiyo ni wale wanaopata uchungu
kupitiliza,kuchelewa kujifungua,kushindwa ama wa kutoka jamii tofauti na
wafugaji wa kimasai ambao hata hivyo ni wachache katika kata hiyo na
kata jirani ambazo nyingi hupata huduma kwenye zahanati hiyo.
Bibi Miriam amekanusha usemi wa baadhi
ya watu ya kuwa kisa cha wamama hao kujifungulia majumbani ni kuficha
kutambulika ya kuwa wamekeketwa, akisema kuwa wao hawajishughulishi na
jambo hilo tofauti na kuwashauri juu ya madhara yatokanayo na
ukeketaji wakati wa kujifungua.
Hata hivyo amewataka wakunga wa jadi
ambao wanaonekana kuwa chanzo kingine cha akina mama kuto jifungulia
Zahanati kuacha kuwazalisha wa mama hao majumbani, badala yake
wawashauri na kuwapeleka kujifungulia katika zahanat na vituo vya afya,
na wao kujifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza wakati wa matukio hayo.
0 Comments