Advertisement

Responsive Advertisement

Mke wa Mtu Asaula Nguo Akimfuta Jasho Bi. Harusi

Mwanamke mmoja ambaye inadaiwa ni mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la Mishi Choggo ametoa kali ya mwaka baada ya kusaula kisha kutumia gauni lake kumfutia jasho bi. harusi.
 
Bi’mkubwa huyo alifanya kioja hicho Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Rose Garden maeneo ya Mafinga mkoani Morogoro katika harusi ya Rose Raphael na Edward Sebastian ambao walikuwa wakibariki ndoa.
mke
 
Wakati sherehe ikiwa imepamba moto na waalikwa mbalimbali wakianza kutoa zawadi, mama huyo alimfuata DJ na kuomba awekewe wimbo wa taarabu, akaanza kucheza kwa madaha huku akienda kutunza.
  
Mama huyo alipomkaribia bibi harusi, alisaula gauni lake refu na kulitumia kumfuta jasho bi. harusi baada ya kukosa hanjifu.
 
Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu wanaojiheshimu kuinamisha vichwa chini kwa aibu huku wale micharuko wenzake wakishangilia

Post a Comment

0 Comments