Baada
ya kudaiwa kulipwa fedha na kuingia mitini kwenye matamasha mbalimbali,
mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando
(pichani) amenaswa akitumbuiza jukwaani akiwa na ujauzito mkubwa.
Tukio
hilo lililowashangaza watu wengi lilitokea Jumapili iliyopita katika
Kijiji cha Ilongero jimbo la Singida Kaskazini kulipokuwa na mkutano wa
hadhara aliokuwa akiuhutubia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu.
Wakati
wananchi wakimsubiri Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa Singida Kaskazini
ahutubie, zilitangulia burudani za hapa na pale ndipo baadaye
alipopanda Rose akiwa na kitumbo ‘ndii’ na kusababisha minong’ono chini
kwa chini.
“Mh!
Jamani huyu ni Rose kweli au macho yangu? Si angepumzika? Mbona tumbo
tayari kubwa hivi, hata kama ni kusaka pesa lakini si kwa staili hii,
kuna wakati mtu inabidi fedha uzipe kisogo,” alisikika mmoja wa wananchi.
Hata
hivyo sambamba na watu kutilia shaka juu ya afya yake, Rose alionekana
kulimudu vyema jukwaa kwa kutumbuiza nyimbo zake huku akiimba kwa staili
ya kurukaruka kama kawaida.
Kwenye
mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Ilongero na jimbo zima
la Singida Kaskazini, mbali na kuzungumzia masuala mbalimbali ya
maendeleo, Nyalandu alitangaza nia ya kugombea urais mwakani.
0 Comments