Staa
wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ amemshauri msanii mwenzake,
Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupigania kuolewa na mwandani wake, Nuhu
Mziwanda ambaye alimvisha pete ya uchumba siku chache zilizopita kwa
kuwa kitendo hicho kwa sasa kimeshazoeleka.
Akiongea
na mwandishi wetu, Sandra alisema anafagilia sana mapenzi ya wawili hao
kwani anaona wanaendana pamoja na utofauti wa umri uliopo anamtaka
Shilole ahakikishe anaolewa haraka iwezekanavyo kwani hata mwanadada
Wema Sepetu alivishwa pete ya uchumba na Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ lakini mpaka sasa hawajafunga ndoa malengo yao yameishia
njiani.
0 Comments