Maafisa wa afya katika ufalme wa
Thai wamesema kuwa wavulana ambao wanaogopa kuchagua mipira ya kondomu
zinazowatosha vizuri ndiyo chanzo cha mlipuko wa magonjwa ya zinaa
miongoni mwa vijana.
Katika taarifa ilioambatana na siku ya
wapendanao ya Valentine-siku ambayo maafisa wa Thai hutoa onyo kuhusu
mapenzi ya ujana.
Wizara ya afya ya umma ilionya kuwa magonjwa ya zinaa
miongoni mwa wavulana wa miaka 10 hadi19 yameongezeka mara tano zaidi
katika kipindi cha miaka 10 iliopita.
''Ni kwa sababu ni asilimia
43 ya vijana ndio wanaotumia mipira ya kondomu na kwamba huchagua mipira
ambayo ni mikubwa ikilinganishwa na vipimo vyao huku wakiogopa kwamba
watafanyiwa masikhara kwa kuwa wadogo''.
Wizara hiyo imeongeza
kwamba inapanga kutumia dola millioni 1.4 mwaka huu ili kugawanya zaidi
ya mipira millioni 43 kwa watu wote katika ufalme huo.
Vijana katika ufalme huo hufunzwa kutofanya ngono badala kuambiwa watumie kinga wakati wanapotekeleza tendo hilo.
via>>BBC
0 Comments