WAKATI mvua zikiendela kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, na sehemu
nyingine nchini, wakazi wake wengi wameonekana kuhangaika kupata
sehemu salama za kuishi na kufanyia biashara.Mtandao huu umezungukia
maeneo mbalimbali ya jiji na kukuta wakazi wa maeneo mengi wakitoa maji
kwenye nyumba zao na sehemu za kufanyia biashara.
Wakiongea na mwandishi wetu, wakazi wa maeneo ya Mwanayamala-Mkwajuni
maarufu kama Bondeni, wameitupia lawama kampuni ya ujenzi ya Strabag
kuwa imechangia nyumba zao kuingiliwa na maji kwani mifereji
iliyotengenezwa haikidhi uwezo wa kusafirisha maji kwa kasi kwani ni
midogo na badala yake maji hujaa na kuelekea katika makazi yao.
Katika maeneo ya Jangwani mtandao huu ulikuta baadhi ya nyumba zilizoko
bondeni zikiwa karibu kumezwa na maji, ambapo wakazi wa maeneo hayo
wametaka serikali iwasaidie.
Katika soko la Sinza Afrika-Sana, wafanyabiashara ndogondogo wa soko
hilo wameelezea kero inayosababishwa na mifereji inayopitisha maji
barabarani kuziba kufuatia uchafu unaotupwa ovyo na hivyo kuelekeza maji
katika biashara zao na wateja kukosa sehemu ya kupita.
Vilevile, wafanyabiashara ndongondogo eneo la Ilala-Boma katika soko la
Mchikichikini, wamesema mvua zinazoendelea zinawafanya wengi wao kukosa
fedha ya kujikimu kutokana na wateja kutokufika kwenye vibanda vyao
kwani maji yanajaa sehemu hizo zaq biashara.
0 Comments