Licha
ya kuwepo mauaji ya albino nchini limekuibuka kundi la watu wanao fanya
vitendo vya kuchinja watu shingo na kuondoa koromeo kwa watu wa kawaida
mkoani Kagera limeongeza hofu kwa wakazi wa wilaya za Bukoba mjini,
vijini na Misenyi.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoa wa Kagera wamesema vitendo vya
mauaji ya kikatili ya kuchinja watu shingo na kuondoa baadhi ya viungo
vyao vinasikitisha na kuendelea kuleta hofu kubwa kwa wakazi wa mkoa huo
ambapo wameogeza kwa kulitaka jeshi la polisi kuendelea kuimarisha
ulinzi katika kata ya Kitendaguro, Kibeta na Kagondo na kuhakikisha
juhudi za kukomesha vitendo hivyo zinafanyika.
Mapema
akiongea Kupitia kituo cha ITV kamanda wa jeshi la polis mkoani Kagera
ACP Henri Mwaibambe amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za
kuwasaka wa harifu hao ambapo ameongeza kuwa jeshi hilo sasa
linawashikilia watu nane wanaodaiwa kuhusika na matukio ya kuchinja watu
wasiokuwa na hatia huku akiwataka wananchi kuwa na subira na kutoa
ushirikiana kwa jeshi la polisi ili kwapamoja waweze kudhibiti uharifu
huo.
Hivi
karibuni yametokea matukio ya watu kuchinjwa wa nakuondolewa baadhi ya
viungo vyao katika maeneo ya Kitendaguro na Kibeta Kando na Bugabo
Katoma ambapo katika eneo la Rwamishenye wananchi wenye hasila kali
walijichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mtu hadikufa wakimuhisi
kufanya vitendo hivyo.
0 Comments