NI huzuni tupu! Aliyekuwa mhamasishaji kwa nyimbo wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), mkazi wa Kijiji cha Nyashimo mkoani Simiyu, Bundala Mayala (72),
amekutwa amekufa kwa kunyongwa nyumbani kwake.
Mtoto wa mdogo wa marehemu ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini
alisema, mwili wa baba yake mkubwa uligundulika Februari 25, mwaka huu,
saa nane mchana ambapo ulikutwa na majeraha kadhaa na alipoitwa daktari
kumpima alithibitisha kupoteza maisha kwa kunyongwa.
“Siku hiyo ya mwili kugundulika nilikuwa nakwenda nyumbani kwake baba
mkubwa kwa lengo la kumsalimia, lakini nilishtuka baada ya kukaribia
kwani nilisikia harufu kali ya kitu kilichooza ikitoka ndani huku mlango
ukiwa wazi.
“Nilipofika nilichungulia ndani nikaona mguu wa baba ukiwa umejikunja.
Ndipo nikaingia haraka na kumkuta marehemu akiwa chini, ameegemea
baiskeli yake huku sehemu kubwa ya mwili ikiwa imevimba.“Nilitoka kwenda
kuwauliza majirani ambao nao walibaki wakishangaa kwani hata wao
walikuwa hawajamuona kwa siku mbili.
“Hata hivyo, wanakijiji na wananchi wengine walishtushwa sana na kitendo
hicho kwani marehemu alikuwa ni chombo muhimu sana ndani ya CCM
kutokana na umahiri wake wa kuhamasisha shughuli za chama hicho kwa
kutumia kipaji chake cha uimbaji.“Baada ya hapo, nilikwenda kutoa
taarifa kwa uongozi wa kijiji ambapo viongozi walifika, wakawaita
wanakijiji wote, mimi nikaelekea kituo cha polisi kutoa taarifa,”
alisema mtoto huyo.
HALI YA MWILI
Kijana
huyo alisema kifo cha baba yake kinatatanisha baada ya uchunguzi wa
daktari kuonesha kuwa mishipa ya shingo yake ilikatika, mbavu ziliumia
na sehemu ya kiunoni iliumia huku ulimi akiwa ameung’ata na alimwagiwa
maji ya moto kwani alibabuka na sehemu ya nyama ya haja kubwa
ilinyofolewa.
Aliendelea kusema kuwa, licha ya polisi kufika nyumbani kwa marehemu
lakini mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo na afisa
mmoja wa jeshi hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa
kuwa si msemaji alisema uchunguzi bado unaendelea.Marehemu alizikwa siku
hiyohiyo baada ya kugundulika kufuatia jeshi la polisi kutoa ruhusa.
0 Comments