Kwenye
vituo vingi vya daladala utakuta mida ya jioni wako jamaa wanachoma zao
mishkaki.. na watu wamezoea kabisa unakuta watu wengi wamejipanga
wanajisevia.. kua story ilitokea Temeke kwamba kuna jamaa alikuwa
anatuhumiwa kwamba anauza mishkaki ya paka, ikamharibia biashara yake
japo baadae iligundulika kwamba mishkaki haikuwa ya paka.
Philip Paul kagonga
vichwa vya habari kwenye story za Nigeria, amesema yeye na familia yake
ni walaji wazuri wa mishikaki ya chura na pia ni biashara yake
inayomuweka mjini.. YES.. anauza mishkaki hiyo !!
Philip amesema shughuli ya kukamata vyura hao huwa anafanya usiku, anachotumia ni mikono tu.. wala haimpi shida sana kuwakamata.
Hii
ni biashara yake kubwa, unaambiwa kaianza toka mwaka 2008, sehemu
ambayo huwa anawakamata sana vyura hao ni Jimbo la Adamawa, Nigeria
alafu anawasafirisha mpaka Benue, huko nd’o ambako kuna soko kubwa la
mishkaki hiyo.
0 Comments