Kuna
tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa, lakini leo nimekuja na hii list
ya Marais nane wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa zaidi ya wenzao
Afrika.
Iko ishu ya Marais kung’ang’ania
madaraka kwenye nchi za Afrika, kingine ni hii ishu ya kujilimbikizia
mali, japo wapo wanaokuwa nazo kabla ya kushika madaraka lakini wengine
wanajichumia hapohapo wakiwa madarakani.
Jose
Eduardo Dos Santos ndiye Rais anayeongoza kwa utajiri Afrika. Ni Rais
wa Angola, aliingia madarakani mwaka 1979, utajiri wake ni dola bilioni
20
Mohammed VI- Ni Mfalme wa Morocco ambaye amekaa madarakani kwa miaka 15, ana utajiri wa dola bilioni 2.
Teodoro Obiang Nguema Mbasogo: Huyu
ni Rais wa Equatorial Guinea, aliingia madarakani 1979.. ana una
utajiri wa dola milioni 600. Nchi yake ni moja ya nchi ambazo ni maskini
sana lakini huo ndio utajiri wake mwenyewe.
Uhuru Kenyatta ni
Rais wa Kenya. Kaingia madarakani mwaka 2011, utajiri wake ni dola
milioni 500. Mbali ya kuwa Rais ana miradi mingi pamoja na hisa kwenye
Mabenki makubwa na mahoteli ya kifahari.
Paul Biya ni
Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ana utajiri wa dola milioni 200,
unaambiwa ndiye rais anayetumia kiasi kikubwa cha pesa katika ziara zake
kuliko marais wote duniani. Ziara yake kwa siku moja ni kama Euro
30,000 hivi.
King Mswat iii Ni
mfalwe wa Swazland akiwa na utajiri wa dola milioni 100, anashika
nafasi ya 15 katika familia za kifalme tajiri duniani, Unaambiwa wake
zake 13 hutumia zaidi ya dola milioni sita kufanya manunuzi yao pekee,
pia Serikali yake hutenga bajeti ya dola milioni 61 kila mwaka kwa ajili
ya matumizi ya nyumbani
Idriss Derby Ni Raisi wa Chad tangu mwaka 1990 na ana utajiri wa zaidi ya dola milioni 50
Robert Mugabe wa Zimbabwe, ana zaidi ya miaka 26 akitawala nchi hiyo. Utajiri wake ni dola milioni 10
0 Comments