Gladness Mallya
MTANGAZAJI mkongwe wa
televisheni, Sauda Mwilima ambaye mumewe, Kauli Juma aliondoka mara tu
baada ya kufunga naye ndoa kuelekea Afrika Kusini kikazi, amesema wa
ubani wake huyo amesharejea na hivyo kuwakejeli waliokuwa wakisema kuwa
ndoa yao ilikuwa ni magumashi.
Mtangazaji mkongwe wa televisheni, Sauda Mwilima.
Akipiga stori na
paparazi wetu, Sauda alisema kwa sasa anaifurahia ndoa yake vilivyo
baada ya mumewe kurudi Bongo baada ya kuwa Afrika Kusini kikazi kwa muda
mrefu na baadhi ya watu kuzungumza mengi kuhusu ndoa yao.
“Nadhani watu sasa
watajua kuwa siyo jambo zuri kuzungumzia kitu usichokijua, mume wangu
amerudi na hakuna ninachokifurahia kama ndoa yangu. Ama kweli ndoa ni
tamu,” alisema Sauda.
0 Comments