Advertisement

Responsive Advertisement

WAFANYABIASHARA WASITISHA MGOMO WAO MJINI SONGEA


Wakati mgomo wa wafanyabiashara wa kutofungua maduka ukiendelea mjini Songea mkoani Ruvuma mgomo wa waendesha Daladala uliodumu kwa siku nzima jana umesitishwa.

Mwenyekiti wa wasafirishaji wa mkoa wa Ruvuma Bw.Golden Sanga amesema kuwa wameamua kusitisha mgomo wa Daladala ili kutoa nafasi ya Viongozi kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara huku mgomo wa kutofungua maduka ukiendelea.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Ruvuma Bw.Isaya Mbilinyi amesema kuwa madai yao yasiposikilizwa ya kutatuliwa utata  wa mashine za EFDS,ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja na kuachiwa kwa dhamana mwenyekiti wao wa taifa Bw.Johnson Minja mgomo huo utakuwa endelevu.
 
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu anawasihi wafanyabiashara kusitisha mgomo wao kwa kuwa kuendelea kugoma ni kuwaumiza wasio na hatia bila sababu ya msingi.
 
Wakati hayo ya kijiri huko tayari Mwenyekiti wa wafanya biashara Bwana.Johnson Minja amepewa Dhamana na mahakama Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma.

Post a Comment

0 Comments