Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Rose Ndauka sasa Ndauka
kwa sasa anadaiwa kuzama kwenye penzi zito la Prodyuza wa Bongo Fleva,
Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’ hii ni baada ya mahusina na mzazi
mwenzie, Malick Bandawe kuvunjika.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kwa muda mrefu wawili hao
wamekuwa wakionekana sambamba kama kumbikumbi hasa nyakati za usiku
katika maeneo tofauti ikiwemo studio ambayo Manecky anafanyia kazi zake
na sehemu nyingine.
“Rose na Manecky ni wapenzi kwani muda mwingi wako
pamoja, wanaongozana kama kumbikumbi hasa usiku.
Huwa tunawaona wanakuja
maeneo ya hapa Afrika Sana wanakwenda kununua chakula cha jioni huku
Manecky akijinadi kuwa ameamua kuwa na Rose kwa kuwa mke wake halali
hivi sasa ni mjamzito,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi aliwatafuta wawili hao ili kuweza kujibu tuhuma hizo ambapo Manecky
alipopatikana alikanusha na kudai ukaribu wao unaletwa na kazi.
“Ukaribu wangu mimi na Rose ni kazi tu kwani kuna ‘project’
tunaifanya nadhani mwenyewe Rose ndiyo anaweza kuweka wazi hilo, kingine
Rose anafanya kazi na mdogo wangu kwenye gazeti la Rozzie la
mtandaoni,” alisema Manecky.
Alipoulizwa kama ameamua kutembea na Rose kwa sababu mkewe ni
mjamzito, Manecky alizidi kusisitiza kuwa si kweli.
“Hamna kitu kama
hicho jamani.” Ili kupata upande wa pili, mwanahabari wetu alimvutia
waya Rose ili kujua anazungumziaje tuhuma hizo likiwemo suala la
kuonekana na Manecky mara kwa mara, naye aliruka viunzi:
“Hakuna kitu kama hicho jamani, kwani mimi nachaguliwa mtu wa kukaa
naye? Acheni kusikiliza maneneo ya watu halafu Manecky ana mke ambaye ni
mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote,” alisema Rose.
Rose na
Malick kabla ya kumwagana miezi michache iliyopita, walidumu kwenye
uhusiano kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.
0 Comments