Ni
binti mrembo wa miaka 21 aliyefikia Chuoni kimasomo ambapo alichukua
maamuzi ya kununua dawa za kupunguza/kujikinga na unene alizozinunua
kwenye mtandao (online).
April
12 2015 ndio ilikua siku yake ya mwisho duniani baada ya kulazwa
hospitali na chanzo cha kifo chake kikiaminika ni hivyo vidonge ambavyo
inasemekana vilikua na sumu.
Mama
yake mzazi ameongea na kusema Madaktari wasingeweza kuokoa maisha yake,
kunywa hizo dawa ni sawa na kujisogeza karibu na kifo, zinasababisha
pia mwili upate joto kupitiliza na kusababisha pia ini kushindwa kufanya
kazi.
Eloise
alipoanza kuona hali iko tofauti baada ya kunywa dawa alikwenda
hospitali mwenyewe lakini ikawa imeshaharibu tayari, alichelewa kwenda.
Haikufahamika
ni vidonge vingapi alimeza na alivitumia kwa muda gani lakini Polisi wa
Uingereza wametoa onyo kwa yeyote mwenye mpango wa kununua dawa online
aachane nao tena sanasana kupitia websites ambazo hazijasajiliwa.
0 Comments